MAHAKAMA YAMWACHIA HURU MFANYABIASHARA YUSUF MANJI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mfanyabiashara Yusuf Manji (41) na wenzake watatu waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka saba ya uhujumu uchumi na usalama wa Taifa kwa kukutwa na vitambaa vinavyotengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyenye thamani ya zaidi ya Sh 200 milioni na mihuri.

Mbali na Manji wengine walioachiwa huru ni Deogratius Kisinda(28), Abdallah Sangey(46) na Thobias Fwere (43).
Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi leo Alhamisi amewaachia huru washtakiwa hao saa saba mchana mara baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kuomba ifutwe kwa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendeleza mashtaka hayo dhidi ya washtakiwa hao na Mahakama ikaridhia.

No comments:

Post a Comment