Dar es Salaam. Msanii maarufu wa kike wa fani ya uigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael Kimemeta, maarufu kama Lulu, anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya aliyekuwa msanii maarufu wa kiume wa fani hiyo, Steven Kanumba, keshokutwa atapanda kizimbani tena wakati kesi hiyo itakapoanza kuunguruma.
Lulu ambaye yuko nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akidaiwa kumuua Kanumba bila kukusudia, kinyume cha Kifungu cha 195 cha Kanuni za Adhabu (PC), April 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican.
No comments:
Post a Comment