MAHAKAMA YAIDHINISHA USHINDI WA KENYATTA KENYA

Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya imetupilia mbali kesi mbili zilizowasilishwa kwa nia ya kutaka kufutwa matokeo ya uchaguzi wa mwezi Octoba.

Majaji wanaosikiliza kesi hizo wanasema hapakuwa na ushahidi wa kutosha kufuta uchaguzi huo .

Baada ya kutupwa kwa kesi hizo zoezi la maandalizi ya kumwapisha Rais Uhuru Kenyatta tarehe 28 mwezi November mwaka huu limeanza.

Wafuasi wa chama cha Jubilee waliokuwa nje ya Mahakama ya juu zaidi wameonekana wakiingia mitaani kushangilia uamuzi huo wa Mahakama .

Mitaa mbalimbali ya Nyeri , Gatundu na Eldoret imelipuka kwa shamrashamra za furaha ya uamuzi huo wa Mahakama.

No comments:

Post a Comment