Lysa Bantu katibu wa kamati iliyoratibu mkutano wa kurudisha Jumuiya ya waTanzania DMV akifungua mkutano uliofanyika Jumapili Januari 14, 2018 Mt. Rainier, Maryland na kuhudhuriwa na wanaDMV wapatao takribani 100 ambao waliwachagua kamati itakayoipeleka DMV kwenye uchaguzi mkuu, waliochaguliwa kwenye kamati ya uchaguzi ni Julius Manase, Richard Mawenya, Eddah Gachuma, Jessica Mushala, Abdul Simba, Robert Saulanga na Kenyatta Mayanga. Kamati iliyoratibu mkutano huo iliyoongozwa na Mwenyekiti Rebeca Ndekeja, Lysa Bantu Katibu, Musa Shedafa naibu katibu, Jabir Jongo, Mweka hazina, Emmanuel Nnko mweka hazina msaidizi, Wajumbe wa kamati ni Said Mwamende, Joha Nyang'anyi, Julia Nyerere, Mponi Atu, Lucas Moshi, Lilian Mnzava na Benjamin Mwaipaja. PICHA NA VIJIMAMBO BLOG NA KWANZA PRODUCTION.
Mwenyekiti wa kamati Rebeca Ndekeja akielezea jambo na kuwashukuru Said Mwamende na Jabir Jongo (hawapo pichani) kwa wazo lao la kufufua jumuiya baada ya kutokua hewani kwa takribani miaka miwili.
Kutoka kushoto ni Mponi Atu, Emmanuel Nnko, Julia Nyerere, Rebeca Ndekeja, Lysa Bantu, Joha Nyang'anyi na Said Mwamende.
Naibu Katibu Musa Shedafa ambaye ndiye aliyekua mshereheshaji wa mkutano huo.
Dr. Hamza Mwamoyo mkuu wa idhaa ya kiswahili VOA ambaye alishiriki kutunga katiba ya DMV akifafanua jambo kuhusiana na katiba hiyo ya DMV.
professor Boas akielezea jambo
Given ambaye pia alikua mmoja wa waliounda katiba ya DMV akifafanua kifungu cha katiba.
Mwang'ombe "Bagassa" Libe akichangia jambo.
Hamza naye akichangia jambo.
Kamati ya uchaguzi ikipata picha ya pamoja na kamati iliyoandaa mkutano wa kufufua DMV.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
No comments:
Post a Comment