Msanii wa Bongo Flava, Diamond Platnumz amenusurika katika ajali ya gari nchini Marekani ambapo yupo kwa ajili ya tour ya albamu yake ‘A Boy From Tandale’
Muimbaji huyo amepata ajali hiyo wakati akitokea kwenye show. Kupitia mtandao wa Instagram ameandika;
"Dah Tumepata ajali na kunusurika kufa usiku wa leo wakati tunatoka kwenye show….ila Mwenyez Mungu ametupa nafasi nyingine tena ya kuishi na kuendelea kushikana mkono na vijana wenzangu mtaani kwa pamoja tuziokoe familia zetu duni…."
Diamond ndiye mwanzilishi na mmiliki wa label ya WCB ambayo inasimamia wasanii kama Harmonize, Rayvanny, Rich Mavoko, Queen Darleen, Lava Lava na Mbosso.
No comments:
Post a Comment