TANZIA: MHASIBU MKUU BUGANDO HOSPITAL, AJIUWA KWA KUJIRUSHA GOROFANI

Mkurugenzi wa Fedha na Mipango katika Hospitali ya Rufaa Bugando ya jijini Mwanza, mtawa Suzan Bathlomeo amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka gorofani muda mfupi baada ya kutoka kusali misa ya saa 12:00 asubuhi, leo Jumanne Agosti 28, 2018.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa taarifa kamili atazungumza na waandishi wa habari baadaye.

Kwamjibu wa Ofisa Uhusiano wa Bugando, Lucy Mogele amesema mtawa huyo amefariki dunia leo alfajiri, huku akibainisha kuwa hospitali hiyo haina mamlaka ya kuzungumziwa suala hilo na kutaka litafutwe shirika la watawa la Kagera, ambalo makao makuu yake yapo mjini Bukoba mkoani Kagera.

No comments:

Post a Comment