KILICHOTOKEA MAHAKAMANI RUFAA YA MBOWE NA MATIKO

LEO Jumatatu, Februari 18, 2019 kesi ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko kuhusu mapingamizi ya serikali dhidi ya kesi yao ya kupatiwa dhamana imesikilizwa kuanzia asubuhi katika Mahakama ya Rufani.


Upande wa Mashtaka umewasilisha hoja mbili za rufaa katika Mahakama hiyo huku wakiomba rufaa hiyo iliyopo Mahakamani hapo mbele ya Jaji Sam Rumanyika itupiliwe mbali kwa sababu haiendani na kifungu cha 362 (1) cha sheria ya Makosa ya Jinai sura ya 20 iliyofanyiwa marejeo.

Kwa mujibu wa sheria hiyo rufaa ni lazima iambatanishwe na mwenendo wa kesi na uamuzi mdogo unaobishaniwa katika Mahakama Kuu lakini upande wa utetezi hawakufanya hivyo.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, akitoka katika Mahakama ya Rufaa kusikiliza rufaa ya kesi ya mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Mbunge Esther Matiko.

Rufaa hiyo ilikatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) dhidi ya Mbowe na Matiko akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu, kukubali kuendelea na usikilizwaji wa rufaa ya wabunge hao ya kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana.

No comments:

Post a Comment