BREAKING NEWS: DKT. REGINALD MENGI AFARIKI DUNIA DUBAI

Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi, enzi za uhai wake.

MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt Reginald Abraham Mengi (75) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Mei 2, 2019 akiwa jijini Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).

Mengi alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa barani Afrika, ambapo sehemu ya utajiri wake aliuelekeza kwa jamii kwa kutoa misaada mbalimbali. Kwa mujibu wa jarida la Forbes mwaka 2014, utajiri wa bilionea huyo ulitajwa kuwa ni TZS trilioni 1.3 (Dola 560 milioni).

Alizaliwa mwaka 1944 mkoani Kilimanjaro na amefariki ikiwa ni miezi sita tangu kufariki kwa aliyekuwa mke wake, Mercy Mengi.

Aliwahi kushinda tuzo mbalimbali za kitaifa na kimataifa, na aliandika kitabu ‘I Can, I Must, I will’.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina!

No comments:

Post a Comment