MAFISADI WA IPTL KUANIKWA NOV 26


HATIMA ya vigogo wanaotuhumiwa kuchota fedha zaidi ya sh. bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), itajulikana Novemba 26 mwaka huu, wakati ripoti ya uchunguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), itakapowasilishwa bungeni na kujadiliwa.
Hatua hiyo ni baada ya Bunge kutuliza munkari wa wabunge kwa kuthibitisha kwamba hakuna barua yoyote iliyowasilishwa na Jaji Mkuu ili kuzima mjadala wa ripoti hiyo kama ambavyo imekuwa ikidaiwa.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Hassan Zungu, wakati akitoa mwongozo wake kuhusu madai kwamba Mahakama imeandika barua kwenda ofisi ya Spika kuzuia mjadala wa kashfa ya IPTL.
Mwongozo wa Zungu, ulitokana na kauli ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Moses Machali, kuhusu azimio la…


No comments:

Post a Comment