Ndg wanafamilia na wanaukoo wa One Martin One Family, TYK:
Kwa niaba ya mpendwa Mzee wetu Baba Lucas Martin Mushi (a.k.a Baba Fortu ) anapenda kuwasilisha kwenu taarifa ifuatayo:-
Kwa mapenzi ya Mungu Mnamo siku ya Jumapili tarehe 28 mwezi wa 12 mwaka 2014 kutakuwa na ibada ya Misa takatifu kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kuwajalia kuadhimisha miaka 50 ya ndoa.
Ibada ya Misa takatifu inatarajiwa kufanyika katika Parokia ya Karanga iliyopo wilaya ya Moshi.
Kwasababu hiyo ambayo ni ya kumpendeza Mungu wazee wetu wapendwa Baba na Mama Lucas wanatumia fursa hii kukukaribisha rasmi na tuwasindikize na kushiriki pamoja katika ibada ya Misa takatifu. Ibada hii itaanza saa 4:30 asubuhi.
Kwa taarifa hiyo unaombwa kuitenga na kujiandaa kwa siku Jumapili ya tarehe 28-12-2014 Kwa ajili ya tukio hilo muhimu kwani uwepo wako ni muhimu sana!
Ratiba na utaratibu wa matukio baada ya ibada itawasilishwa punde!!
TYK
No comments:
Post a Comment