LIKIZO MNAENDA BUSH AU MNAKIMBILIA DAR?


MADENTI mambo vipi? Tunakutana tena katika wikiendi nyingine ambayo wengi wenu inawakuta mkiwa likizo. Ni kipindi cha kwenda kuwatembelea ndugu, jamaa na marafiki popote walipo. Kipindi hiki kinanikumbusha sana mambo ya enzi zile aisee, yaani wakati wa likizo ni full purukushani. Wakati huo, wengi walikuwa wanakimbilia kwenda Dar, si unajua tena mimi nilisoma mkoa, kwa hiyo kipindi kama hiki kikifika, ni shiida!
Waliokuwa wanakwenda likizo Dar walikuwa wanatisha, manake ndiyo walionekana wajanja, wanaofaidi maisha. Sijui hivi sasa ikoje, lakini kama utaniuliza mimi sasa hivi ningepata likizo nitakwenda wapi, ningekuambia naenda zangu bush aisee.
Unajua kwa nini? Zamani mzee wetu alitulazimisha kwenda kijijini wakati wa likizo. Yeye alitaka twende tukamsalimie bibi (mama yake)…

No comments:

Post a Comment