INGEKUWA MIMI WEREMA, NISINGESUBIRI KUTIMULIWA, NINGEJIUZULU


Jaji Frederick Werema akizungumza jambo.
Kwako Jaji Frederick Werema.

Najua katika siku za hivi karibuni umekuwa katika wakati mgumu sana kutokana na kushiriki kwako kwa namna moja au nyingine katika sakata la mabilioni ya Escrow. Najua jinsi ulivyochanganyikiwa lakini sina namna nyingine zaidi ya kukufikishia ujumbe huu, hata kama utakuchukiza.
Mimi sikuzaliwa Oktoba 10, 1955 kama wewe. Sikusoma Shule ya Msingi Wegero wala Sekondari za Bwiru na Songea Boys kama wewe. Sikuchukua Shahada ya Sheria pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuhitimu mwaka 1984 kama wewe kabla ya kwenda Amenican University, Washington kuchukua Shahada ya Uzamili na kuhitimu mwaka…

No comments:

Post a Comment