Dar
es Salaam. Tanzania imepoteza kiasi cha Dola 462 milioni za Marekani
(sawa na Sh794.6 bilioni) mwaka 2013 kutokana na rushwa, udanganyifu katika
ankara za malipo na ukwepaji wa kodi.
Shirika
la Kimarekani la Uchumi (GFI) limetoa ripoti mpya na kusema kuwa Tanzania
imepoteza jumla ya Dola 1,762 milioni kuanzia mwaka 2011 hadi 2013.
Ripoti
hiyo iliyotolewa Desemba mwaka huu, inaonyesha kuwa Tanzania imekuwa sugu kwa
kupoteza kiasi kikubwa kila mwaka na kwa mwaka 2010, kiasi cha Dola 1,356
milioni kilipotea wakati Dola 613 milioni zilipotea mwaka 2011 na Dola 717
milioni mwaka 2012.
Waziri
wa Fedha, Saada Mkuya alisema tatizo la udanganyifu katika ankara za malipo
ndilo lililotawala zaidi nchini na kusema linafanyiwa kazi na mamlaka
husika.
Mkuya
alisema Tanzania inapoteza fedha nyingi zaidi kutokana na udanganyifu katika
ankara za malipo ya kibiashara, mchezo ambao umekuwa ukifanywa na raia wa China
ambao ankara zao za malipo huonyesha kuwa wameingiza mzigo mkubwa nchini lakini
ukifika katika Bandari ya Dar es Salaam, huonekana mzigo kidogo.
No comments:
Post a Comment