Wagonjwa wakimtia adabu Mganga Mkuu wa Kituo
cha Afya cha Nyakabale mkoani Geita, Josephat Msafiri baada ya kuwatelekeza
juzi. Picha Jackline Masinde
Geita. Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Magreth Nakainga amemvua madaraka
Mganga Mkuu wa Zahanati ya Nyakabale, Josephat Msafiri kwa kukiuka miiko ya kazi
yake na kulewa wakati wa kazi.
Mkurugenzi
huyo aliamua kuchukua uamuzi huo jana kutokana na tukio lililotokea Juzi hii la
daktari huyo kufunga kituo cha afya na kuacha wagonjwa wakiwa wamezidiwa, kisha
kwenda kunywa pombe jambo lililowalazima kumchapa viboko akiwa baa.
“Tumeshamchukulia
hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kumvua madaraka yake ili iwe fundisho kwa
watumishi wengine wa Serikali,” alisema Nakainga.
No comments:
Post a Comment