Aua, ajiua, aacha ujumbe wa kurasa nne

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela akiwaonesha wandishi wa habari ujumbe ulioachwa na marehemu Emmanuel Moshi baada ya kumuua mfanyabiashara mwenzake Didas Alphonce kwa kumkata na shoka kichwani na kisha yeye kujiua kwa kujinyonga. Picha Joyce Joliga

Songea. Mfanyabiashara wa mbao Manispaa ya Songea, Emmanuel Moshi (40), mkazi wa Marangu, mkoani Kilimanjaro amemuua mfanyabiashara mwenzake aliyetambuliwa kwa jina la Didas Alphonce (64), mkazi wa Kilema Kilimanjaro kwa kumpasua kichwa kwa shoka, kisha yeye mwenyewe kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani katika stoo ya nyumba waliyokuwa wakiishi.
Inadaiwa kuwa Moshi alichukua uamuzi huo baada ya Alphonce kumdhulumu zaidi ya Sh87.4 milioni.
Wakizungumza na gazeti hili jana, watu wa karibu na wafanyabiashara hao ambao hawakupenda majina yao kuandikwa kwenye gazeti, walidai kuwa wafanyabiashara hao walikuwa wakiishi nyumba ya ndugu yake, Didas na kufanya biashara za kuuza mbao pamoja.

No comments:

Post a Comment