Watuhumiwa wa kesi ya kupokea rushwa kutoka
kwenye akaunti ya Tegeta Escrwo, Rugonzibwa Mujunangoma (kushoto) na Theophil
Bakwea na wakiingia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa ajili ya kufunguliwa
mashitaka. Picha na Said Khamis
Dar
es Salaam. Miezi michache baada ya kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow
kutikisa nchi, watumishi wawili waandamizi wa Serikali wamefikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakituhumiwa kupokea rushwa ya
mamilioni ya fedha zilizotoka kwenye akaunti hiyo.
Mahakama
hiyo ilielezwa jana kuwa Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma aliwekewa kiasi cha Sh323
milioni kupitia akaunti yake namba 00120102602001.
No comments:
Post a Comment