Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Jafari
Mohamed.
Watu 13 wanasadikiwa kufa maji katika Ziwa Tanganyika, baada ya meli ya Mv
Mbaga kuzama katika ziwa hilo usiku wa kuamkia Jumapili.
Tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Kala, kilichopo mkoani Rukwa wakati meli hiyo ikitokea Mpulungu, Zambia kuelekea Burundi.
Mwakilishi wa meli hiyo mkoani Kigoma, Juliana Zakenda, alisema meli hiyo ilikuwa imebeba wafanyakazi 14 na tani 437 za mahindi.
Alisema kati ya wafanyakazi hao, ni mmoja tu alieokolewa huku hali yake ikiwa mbaya.

No comments:
Post a Comment