Rais Obama akizungumza na mfalme mpya wa
Saudia, Salman bin Abdul Aziz huko Riyadh, Jan 27,2015
Rais Obama na mkewe Michelle wakiwa na mfalme
Salman huko Riyadh
Rais wa Marekani, Barack Obama alisafiri kwenda Saudi Arabia jumanne kutoa heshima zake kufuatia kifo cha wiki iliyopita cha mfalme Abdullah wa nchi hiyo aliyekuwa na umri wa miaka 90.
Bwana Obama alisimama muda mfupi katika mji mkuu Riyadh, huku akiongoza ujumbe wa watu 30 ambao ulijumuisha maafisa na wabunge pamoja na maafisa waandamizi kutoka utawala wa marais waliotangulia. Akiwa mjini Riyadh, Rais Obama alikutana kwa mara ya kwanza na mfalme mpya wa Saudi Arabia, Salman bin Abdulaziz kabla ya kuondoka nchini humo.
No comments:
Post a Comment