Unga
na bomba
Kasisi mmoja raia wa Australia amefichua na
kuthibitisha kuwa kuna idadi kubwa ya wafungwa wenye asili ya Afrika katika
magereza ya Hong Kong, wengi wao wakiwa ni kutoka Tanzania. Kasisi huyo John
Wortherspoon ambaye kwa sasa anafanya ziara maalum Tanzania, amesema yeye ndiye
ambaye amekuwa akisambaza barua zinazodaiwa kuandikwa na wafungwa wanaoshikiliwa
kwenye magereza hayo ambapo baadhi yao wametaja majina ya watu wanaodaiwa kuwa
wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya waliowatuma kusafirisha dawa hizo.
Padre Wotherspoon amefika kuonana na familia za wafungwa hao pamoja na idara za
serikali zinazohusika na mapambano dhidi ya biashara hiyo hatari ya dawa za
kulevya. Mwandishi wetu Ben Mwang'onda anasimulia zaidi kutoka Dar Es
Salaam.
No comments:
Post a Comment