UVIMBE KATIKA VIFUKO VYA MAYAI (OVARIAN CYST)

Hii ni hali ya mkusanyiko wa maji kuzunguka kifuko cha mayai. Ni ngozi laini na nyepesi juu ya kifuko cha mayai. Kifuko cha mayai huwa kinachipua vifuko vidogovidogo ‘Follicles’ na endapo follicles hizi zitakuwa na ukubwa zaidi ya sentimeta mbili, basi ndiyo huitwa Ovarian Cyst. Uvimbe unaweza kuwa na ukubwa kuanzia saizi ya punje ya njegere hadi saizi ya ukubwa wa chungwa.
Aina nyingi ya uvimbe huu huwa hauumi na hauwi saratani na huweza kutokea na kupotea ingawa unaweza kuwa mkubwa zaidi. Ovarian Cyst huwatokea wanawake wa umri wote kuanzia watoto wachanga hadi mwanamke anapofikisha umri wa kuzaa. Uvimbe pia hutokea hata kwa wanawake waliokoma hedhi. Baadhi ya aina hizi za uvimbe huleta matatizo mfano kuvuja damu na maumivu makali au kugeuka kuwa kansa.
Endapo uvimbe utakuwa mkubwa…

No comments:

Post a Comment