WACHOTA MAJI "TAKA" KWA MATUMIZI YA NYUMBANI

Mama huyu mkazi wa Mabibo jijini Dar es Salaam, akichota maji yanayovuja kutoka kwenye bomba la la maji ambayo hata hivyo yamechanganyika na maji taka yanayotiririka kama yanavyoonekana kutoka kupande wa juu kushoto wa picha hii iliyopigwa Jumanne Aprili 15, 2015. Uchunguzi wa K-VIS blog umebaini kuwa maeneo ya Mabibo na Kigogo, yanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji ambapo sasa wakazi wake hususan akina mama na watoto wamekuwa wakiyatafuta hata yanapoonekana yakiwa kwenye mazingira ya uchafu, ambapo wengine wameonekana wakichota kwenye mitaro ya kupitishia maji machafu
Hapa ni barabarani eneo la Kigogo Randa Bar
Barabarani Randa Bar Kigogo
Mtaroni eneo la Mabibo
K-VIS Blog

No comments:

Post a Comment