SHOGA MWANAUME HAKOMOLEWI


Haya weee, mimi nipo poa unashangaa nini kujibu majibu ya kisasa, mbona hujishangai wewe mama mtu mzima kushindana kwenda utupu na binti yako, sasa likiharibika nani amkanye mwenzake. Hebu nipishe huko ushaanza kukunja domo kama dege lililokosewa kumwagwa. Umenuna umecheka habari ndiyo hiyo.
Leo, shoga yangu nazungumza na wewe mwanamke usiye na haya usiyejua wakati gani wa kumkomoa mumeo, jamani wanawake wengine sijui tumerogwa na mchawi aliyeturoga kaugua wendawazimu sijui nani wa kutuponya.Kuna kitu kimoja jana kilinikera na kunifanya niwarudishe kwenye unyago, nikiwa nakwenda zangu mjini nilipanda kwenye daladala na kukaa siti ya nyuma, mbele yangu kulikuwa na wanawake wawili waliokuwa wakiongea mambo ya ndani bila aibu.
Kutokana na maongezi yao ndiyo maana nikajiuliza kama waliochezwa…

No comments:

Post a Comment