FAHAMU KUHUSU UVIMBE KWENYE OVARI KWA MWANAMKE

MSOMAJI karibu tena kwenye ukurasa huu ambao tumekuwa tukipeana elimu juu ya matatizo mbalimbali ambayo yanaisumbua jamii yetu na ulimwengu kwa jumla.
Leo ningependa nitoe utangulizi wa mada ambayo itakuwa ikiwekwa katika ukurasa huu kwa majuma kadhaa yajayo. Mada yenyewe inahusu tatizo la uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovari).Watu wengi wamekuwa wakisikia wengine yamewakuta na wengine hawajui lolote kuhusu tatizo hili. Niweke wazi kwamba katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kuna uvimbe mwingi ambao hutokea sehemu mbalimbali katika mfumo wao wa uzazi.
Kila sehemu ambayo uvimbe hutokea kuna sababu zake na dalili zake.Hivyo, ni vema unapofanyiwa uchunguzi hospitali ukaambiwa una uvimbe kwenye kizazi ni vema ukauliza uvimbe huo upo sehemu gani ili upate uelewa zaidi wa tatizo…

No comments:

Post a Comment