
Ivan (kulia) akiwa na mpambe wake King Lawrenc (kushoto) na Jose Chameleone.
Ulimwengu una maajabu mengi na mitandao ya kijamii inatusaidia kuyafahamu. Uhusiano wa Diamond na Zari the Bosslady haujawahi kupokelewa vizuri na ex wake Ivan aliyezaa naye watoto watatu wa kiume.
Watoto hao wameendelea kuwa karibu na wazazi wote wawili.
Uhusiano wa ulipoanza tu, Ivan kupitia mpambe na rafiki yake wa karibu, King Lawrenc walianzisha vita kwenye mitandao ya kijamii kuwashambulia Diamond na Zari. Hakuna shaka kuwa Ivan amekuwa akionesha hisia zake za kutoupenda uhusiano wao kupitia Lawrenc ambaye amekuwa akiwashambulia mfululizo.
Katika kipindi ambacho tension kati ya Diamond na Alikiba zimefika kileleni hususan kipindi cha kuelekea tuzo za KTMA 2015, Ivan mwenyewe pia alishiriki katika kampeni za kumuombea kura Alikiba. Ni wazi kuwa Ivan bado hajakubali yaishe, na kumuona mke wake wa zamani akiwa na furaha na Diamond ni kitu kinachomkera zaidi.
Na sasa wakati uhusiano wa Diamond na Zari upo katika kilele cha furaha baada ya kujaaliwa mtoto wa kike, Latiffah, kambi ya Ivan kupitia mpambe wake Lawrenc imedhamiria kuitilia doa furaha hiyo.
King Lawrenc ameanza kutupa mashambulizi kwa Diamond na kueleza kile anachoamini kuwa Tiffah ni mtoto wa Ivan! Kwa historia ya kile Lawrenc amekuwa akikisema tangu mastaa hao waanzishe uhusiano, ni wachache wanaoweza kuamini ‘upuuzi’ huu lakini kiukweli hiki ni kitu kinachoweza kuwakosesha raha Diamond na Zari, kama wakiamua kumjali.
No comments:
Post a Comment