MAKOSA YA KIMTANDAO NA HUKUMU ZAKE


Jamani wana group, naomba niwakumbushe kwamba Mhe. Rais Jakaya M. Kikwete ameshasaini Sheria hiyo ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 na inatarajiwa kuanza kufanya kazi rasmi Septemba mosi, mwaka huu.

Sheria hiyo katika eneo la adhabu kwa wahalifu wa mtandao pamoja na wasambazaji wa picha za utupu na ngono, wasambazaji wa taarifa za uongo, za kibaguzi na matusi na watu wengine wanaofanya udanganyifu unaohusu kompyuta, adhabu ni kwenda jela hadi miaka 10 au kulipa faini isiyopungua Sh milioni 50.

Kwa upande wa kusambaza picha za ngono, matusi, uasherati atalipa faini isiyopungua Sh milioni 30 au kwenda jela miaka 10 au vyote. Lakini mtu atakayesambaza picha za utupu atalipa faini isiyopungua Sh milioni 20 au kwenda jela miaka saba au kutumikia adhabu zote kwa pamoja.

Pia kwenye muswada huo mtu ambaye atatoa taarifa, takwimu au maelezo kwa njia ya picha, maandishi, alama au aina nyingine yoyote zikiwa ni za uongo akipatikana na hatia atalipa faini isiyopungua Sh milioni tatu au kutumikia kifungo jela kisichopungua miezi sita au vyote.

Kwa upande wao, Jeshi la Polisi Tanzania, limeanza kuchukua hatua dhidi ya watumiaji vibaya wa mitandao ya kijamii na hadi sasa imekamata watumiaji hao wengi na wako katika hatua ya kuhojiwa na wengine kufikishwa mahakamani.

“Natumia fursa hii kuwaonya watu waache tabia ya kutengeneza ujumbe wa uchochezi, matusi, uongo na uzushi kwa visingizio vya itikadi, dini na siasa kwani Jeshi la Polisi halitovumilia tabia hizo na watakaobainika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria,” alisema msemaji wa jeshi hilo, Advera Bulimba.

Ziko tabia za watu kuandika kwenye mitandao ya kijamii taarifa za uchochezi na uzushi dhidi ya watu maarufu wakiwemo viongozi au taasisi na baadhi yao wanachunguzwa na wakibainika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mfano wa mmoja wa watumiaji mtandao ambao jeshi limebaini ni pamoja na aliendika taarifa za uchochezi kuhusu tukio la ujambazi na mauaji la Kituo cha Stakishari Ukonga jijini Dar es Salaam na sasa anakabiliwa na kesi ya uchochezi mahakamani.

HABARI KAMILI INGIA KWENYE
http://mwanaharakatimzalendo.blogspot.com/2015/08/sheria-ya-makosa-ya-mitandao-kuanza.html

No comments:

Post a Comment