WAFANYAKAZI DARAJA LA KIGAMBONI WAGOMA

Wafanyakazi wa Kampuni ya China Major Bridge Engineering Co. ltd wamegoma kuendelea na ujenzi wa daraja la Kigamboni, wakiushinikiza uongozi kuwalipa madai yao. Miongoni mwa mambo wanayodai ni malipo ya mshahara wa kima cha chini cha Sh. 325,000 kilichotangazwa na serikali pamoja na kuwapatia mikabata ya kazi.

Khamis Mpili, alisema tangu mradi wa ujenzi huo uanze kuna wafanyakazi hawajapatiwa mikataba ya kazi, hali inayosababisha kukosa haki zao za msingi zikiwamo malipo ya likizo, nyongeza ya mishahara, na kuingiziwa fedha za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (Nssf).

“Kuna wafanyakazi wana mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu hawana mikataba ya kazi, tunataka uongozi utupatie stahiki zetu tuendelee na kazi,” alisema Mpili.

No comments:

Post a Comment