Mtoto afanyiwa ukatili wa kutisha

By Rehema Matowo, Mwananchi
Moshi. Mtoto wa miaka 11 anayesoma Shule ya Msingi Shauri Moyo mkoani Kilimanjaro, anadaiwa kuchomwa na pasi ya umeme sehemu mbalimbali mwilini na dada yake, kisha kufungiwa ndani kwa siku tatu mfululizo.
Akizungumza kwenye ofisi za Mwananchi, mtoto huyo (11),  anayesoma darasa la sita alidai kuwa ukatili huo amefanyiwa na dada yake wanayechangia baba.
Alidai kuwa Agosti 6 baada ya kurudi kutoka shule, dada yake alimtuhumu kumuibia Sh30,000 na mafuta ya kupaka.

No comments:

Post a Comment