DC PAUL MAKONDA AFANYA ZIARA YA KUSHITUKIZA KATIKA GEREJI YA WACHINA NA KIWANDA CHA MAFUTA NA SABUNI,

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wafanyakazi wa Gereji ya Spring City Enterprises inayomilikiwa na raia wa China iliyopo Mikocheni B Mlalakuwa  Barabara ya Mwai Kibaki Dar es Salaam leo, alipofika kusikiliza malalamiko yao mbalimbali yakiwemo ya kutokuwa na mikataba ya kazi licha ya kuwa kazini kwa zaidi ya miaka saba. 
Makonda akiangalia kitambulisho dhaifu wanavyotumia wafanyakazi hao ambacho hakiwezi kutumimika kumuwekea mtu dhamana na shughuli mbalimbali.
Ofisa Uhamiaji wa Wilaya ya Kinondoni, Evarist Mlay akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio baada ya kuwepo madai ya baadhi ya wachina kuishi nchini kinyemela.
DC Makonda (kulia), akiangalia bomba la maji wanayotumia wafanyakazi hao kwa kunywa. Hata hivyo wafanyakazi hao walilalamikia maji hayo kuwa si salama kwa kuwa yanatoka eneo la chooni.
Kiongozi wa gereji hiyo, Mr Yu Viangqian (kushoto), akizungumza na wanahabari kuhusu madai ya kuwanyanyasa wafanyakazi wa kitanzania na kutokuwa na mikataba.
Maofisa uhamiaji wakizungumza na kiongozi wa gereji hiyo.
Mmoja wa wafanyakazi wa gereji hiyo, Geofrey Kayanda akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu changamoto mbalimbali zilizopo katika gereji hiyo.
Sehemu ya gereji hiyo inayolalamikiwa.

Na Dotto Mwaibale

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda leo amefanya ziara ya kusitukiza katika Karakana ya kutengeneza magari ya Spring City Enterprises inayomilikiwa na raia wa China iliyopo Mikocheni B Mlalakuwa  Barabara ya Mwai Kibaki na kukumbana na changamoto kadhaa kutoka kwa wafanyakazi wa karakana hiyo.

Moja ya changamoto kubwa aliyoelezwa na wafanyakazi hao ni kutokuwa na mikataba ya kazi na kukosekana kwa huduma zingine anazopaswa kuzipata mfanyakazi.


Wafanyakazi hao walimwambia Makonda kuwa hawana muda wa kupumzika wala malipo ya ziada ikiwa na mazingira ya kazi yasiyo rafiki.


Makonda baada ya kupokea malalamiko hayo aliutaka uongozi wa viwanda hivyo kurekebisha mfumo wao wa kazi ambapo aliwataka watoe mikiataba ya ajira kwa wafanyakazi hao pamoja na kuboresha mazingira ya kazi na maslahi yao.


Akizungumza na wanahabari Kiongozi anaye simamia karakana hiyo ya kutengeneza magari ya wachina, Mr Yu Viangqian alisema hakuna haki yoyote inayokiukwa katika karakana hiyo kwani wao wamejikita zaidi kutoa mafunzo ya ufundi kwa vijana wa kitanzania na ajira.


"Hakuna jambo baya hapa kwetu sisi tunasaidia vijana wengi kupata ajaira" alisema Mr Yu Viangqian.


(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

No comments:

Post a Comment