Ninayo heshima kubwa kukupongeza kwa kuwa Rais wetu wa awamu ya TANO. Ninayo mambo machache ya kukushauri kama Rais wangu na mimi kama mwananchi wako mpenda maendeleo kama kauli mbiu yako ya hapa kazi tu nayo ni kama ifuatavyo la kwanza ni usafirishaji wa abiria wakati wa usiku badala ya mchana kama ilivyo sasa mimi nakuomba na kushauri turudishe utaratibu wa miaka ya nyuma wa kuruhusu mabasi ya mikoani kusafiri usiku badala ya mchana, hii ni kwasababu. Serikali yetu inapoteza mamilioni ya shilling kwa kuwafanya abiria wawe safarini mchana mathlani kila siku mabasi yanaondoka DAR yasiopungua 400 kila basi linabeba abiria wasiopungua 60 kwa wastani hii maana kutoka mikoani kuja DAR ni idadi ni idadi kama hiyo hii ina maana kuwa watu wasiopungua 48000 wako barabarani wamekaa iddle hawafanyi kazi, na kama wastani kila mtu anazalisha TSHS 50,000/= kwa siku akiwa kazini basi tunapoteza jumla ya shs 2.4 bilioni kila siku ambazo tungeziokoa kwa kuwasafirisha abiria hao usiku, maana kama nitaondoka Mbeya saa 12 jioni Dsm nitafika saa 12 alfajiri nitafikia kazi tu na jioni naondoka Dsm saa 12 jioni nafika Mbeya saa 12 alfajiri na kwenda kazini asubuhi hiyo hiyo hapa hakuna nguvu kazi iliyopotea maana nimepoteza usiku tu ambao hata hivyo ningekuwa nimelala nyumbani badala yake nitalala kwenye basi ,hii Itaokoa mamilioni ya shilling ya watu na Taifa kwa ujumla
No comments:
Post a Comment