Wakiwa katika hali ya sintofahamu.
Makongoro Oging’ na Issa Mnally, UWAZI
DAR ES SALAAM: Hatari! Kufuatia kukamatwa kwa wahamiaji haramu wapatao 42 raia wa Somalia na Ethiopia, Kijitonyama jijini Dar, hofu imetanda miongoni mwa raia ambao wanadai jiji hilo si salama.
DAR ES SALAAM: Hatari! Kufuatia kukamatwa kwa wahamiaji haramu wapatao 42 raia wa Somalia na Ethiopia, Kijitonyama jijini Dar, hofu imetanda miongoni mwa raia ambao wanadai jiji hilo si salama.
Wahamiaji hao walikamatwa Jumapili iliyopita, katika nyumba namba 23, Kitalu 47 mali ya marehemu Mohamed Maganga ambayo kwa sasa inakaliwa na mjane, Salma Maganga akiwa pia mjumbe wa shina namba 23.
Wakiingizwa kwenye gari la polisi.
Kwa mujibu wa mjumbe huyo, vyumba ambavyo walikutwa wahamiaji hao alivipangisha kwa Amani Hamis, wiki nne zilizopita na hakujua kama kuna biashara hiyo inaendeshwa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mpakani ‘B’, Kata ya Kijitonyama, Balbo Kalinga amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola pale wanapoona jambo lisilo sahihi ama watu hatari kama hao.
Mashuhuda wakiwa kwenye tukio hilo.
Wiki mbili zilizopita, gazeti hili liliripoti kukamatwa kwa Wasomali na Waethiopia 105 huko Tabata, Dar na hivyo kuzidisha hofu kuwa jiji hilo si salama kutokana na raia wa kigeni kuvuka mipaka na kuingia na kuishi kwenye makazi ya watu.
No comments:
Post a Comment