Tyga amvalisha pete ya uchumba Kylie!

kylie-jenner-18-birthday-party-21-tyga-ffnTyga akiwa na mpenzi wake Kylie Jenner.
HUENDA sikukuu ya Krismasi ilikuwa poa kwa staa wa Hip Hop, Tyga kwa kumvalisha pete mdogo wa mwanamitindo, Kim Kardashian, Kylie Jenner.
RING
Kylie Jenner akiwa amevaa pete hiyo.
Uthibitisho huo umejidhihirisha juzi kati baada ya mashabiki kubaki mdomo wazi kutokana na picha aliyoposti Kylie kwenye ukurasa wake wa Instagram pamoja na ‘Applikesheni’ yake inaoonesha pete ya uchumba.
Katika kurasa zake hizo, Kylie aliandika;
“Kila mwaka katika msimu huu wa Krismasi mama huniandalia zawadi kubwa lakini mwaka huu imekuwa furaha zaidi. Imekuwa spesho kumaliza mwaka huu kwa kusherehekea na marafiki zangu pamoja na familia… lakini kuna zawadi kutoka kwa mtu mmoja muhimu sana kwangu.”
Baada ya kuandika hivyo alimalizia kwa kujitetea, “Hapana, sijachumbiwa!”

No comments:

Post a Comment