WAZIRI KITWANGA: HATUA KALI KUCHUKULIA KWA YEYOTE ATAKAYE KAIDI KULIPISHA GARI LA ZIMAMOTO WAKATI LINAENDA KATIKA TUKIO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha wakati alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Katika ziara hiyo, Waziri Kitwanga aliliagiza Jeshi hilo kumchukulia hatua kali za kisheria kwa yeyote atakaye kiuka kulipisha gari la Zimamoto na Uokoaji wakati linaenda katika tukio lolote la uokoaji pamoja na kuzima moto. Pia aliitaka Jeshi hilo kuongeza kasi ya kukusanya mapato katika vyanzo vyake mbalimbali. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (kushoto) akitoa taarifa ya utendaji wa Jeshi lake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga aliliagiza Jeshi hilo kumchukulia hatua kali za kisheria kwa yeyote atakaye kiuka kulipisha gari la Zimamoto na Uokoaji wakati linaenda katika tukio lolote la uokoaji pamoja na kuzima moto. Pia aliitaka Jeshi hilo kuongeza kasi ya kukusanya mapato katika vyanzo vyake mbalimbali

No comments:

Post a Comment