Musa Mateja
SIKU chache baada ya muigizaji kiwango Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ kutimuliwa katika nyumba aliyokuwa amepanga maeneo ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam kwa kosa la kutolipa bili ya umeme na maji, Jumatano hii, zilipendwa wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ naye alikutana na kimbembe kama hicho kutoka kwa mmiliki wa nyumba aliyokuwa akiitumia kama studio, iliyopo Sinza Mori, Risasi Jumamosi linakuhabarisha.
Kwa nyakati tofauti, chanzo kinasema majirani waliwahi kupanda juu ya uzio wa nyumba hiyo na kutaka kupunguzwa kwa sauti ya muziki, lakini Diamond na madansa wake wamekuwa wakikaidi kwa madai kuwa hiyo ni sehemu ya kazi yao, jambo lililosababisha kuwasiliana na mmiliki wa nyumba hiyo ili amtoe msanii huyo, vinginevyo watamshtaki.
No comments:
Post a Comment