AY: wakati wa kutoka kivyetu umefika


Ambwene-Yesaya-21Rapa mwenye heshima kubwa katika Bongo Fleva, Ambwene Yessaya maarufu kama AY.
Rapa mwenye heshima kubwa katika Bongo Fleva, Ambwene Yessaya maarufu kama AY, amesema muda wa wasanii wa Tanzania na Afrika Mashariki kufanya kazi za kuwatoa kimataifa bila kutegemea kolabo na wenzao wa nje umefika.
AY, aliyetokea Kundi la East Coast Team, ambaye ndiye alifungua milango ya wasanii wa Bongo kushirikiana na wasanii wa nje, ametoa kauli hiyo hivi karibuni alipozungumzia kolabo yake na Diamond Platinumz katika Video ya Zigo Remix ambayo inafanya vizuri katika mitandao na vituo vingi ulimwenguni.
“Hiyo ni ishara tu ya kuonesha kuwa tunaweza tukafanya kitu sisi wenyewe Watanzania au watu wa Afrika Mashariki, tunaweza kutengeneza muziki mkubwa kama wanavyofanya wengine,” anasema AY. Zigo Remix imebaki na mdundo uleule wa kuvutia aliofanya mtayarishaji Nahreel lakini sauti zake zimesimamiwa na Hermy B wa B’Hits Music Group

No comments:

Post a Comment