Video Queen anayeshaini kwenye tasnia ya Bongo Movie, Gift Stanford ‘Gigy mone’.
Na Nyemo Chilongani,
Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Video Queen anayeuza nyago kwenye video mbalimbali Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ yamemkuta mazito kwa kutupiwa matusi mazito baada ya kuweka picha inayomuonesha akiwa amevaa kihasara katika Mtandao wa Kijamii wa Instagram.
Tukio hilo lilitokea juzikati ambapo msanii huyo ambaye amekuwa na desturi ya kutupia picha za nusu utupu mtandaoni, kutupia moja aliyoonekana anavua suruali na kubaki na kibukta kifupi.
Baada ya kutupia picha hiyo, kilichofuata kutoka kwa wafuasi wa mtandao huo ni kumvurumishia matusi mazito ambayo hayaandikiki gazetini huku wengine wakienda mbali kwa kusema atakuwa amelaaniwa.
“Huyu si bure, atakuwa amelaaniwa. Huwezi kuweka picha kama hizi kwenye mitandao ya kijamii kama una malezi mazuri ya wazazi. Ni laana hii inayomsumbua,” aliandika mdau mmoja mtandaoni huku mwenzake akiunga mkono:
“Huyu dada anajiaibisha sana, hii picha si ya kuweka hadharani namna hii, sasa angalia anavyoambulia matusi. Mimi namuonya tu awe makini kwani bado kuna sheria kali za mitandaoni.”
Mara baada ya kushuhudia matusi hayo mtandaoni, gazeti hili lilimtafuta Gigy kwa njia ya simu ambaye alionekana kutoshangazwa na matusi hayo.
“Nawashangaa sana wote wanaonisema kisa picha, mbona ya kawaida sana, yaani kama mtu anashangaa picha kama hiyo, za kina Nick Minaj atasemaje? Kwangu naona picha za kawaida kwani nimevaa nguo ambazo natembea nazo barabarani,” alisema Gigy.
No comments:
Post a Comment