TAARIFA YA MSIBA USA WA DADA JESSIE CHIUME.


TAARIFA YA MSIBA USA WA DADA JESSIE CHIUME.

Jumuiya ya Watanzania New York pamoja na familia ya Marehemu Mzee Kanyama Chiume inasikitika kuwataarifu Msiba wa Dada yetu mpenzi Jessie Wayasa Chiume (maarufu kama Da Mgeni) uliotokea ghafla asubuhi ya Jumatano February 24/2016 kwa ajali ya gari huko Mt. Vernon, NY. 


Jumuiya  ya Watanzania wa New York tunasisitiza ushirikiano katika kufanikisha Msiba huu mzito. Tuungane kuwafariji wanafamilia pamoja na kutoa rambirambi zitakazosaidia gharama za kumpumzisha Dada yetu kama ilivyo desturi yetu. 


Leo hii Ijumaa familia itaendelea kuwapo 44 Fleetwood Ave, Apt 3B, Mt Vernon NY 10552). Kuanzia kesho Jumamosi February 27 msiba utakwenda Poconos, PA nyumbani kwa Kaka mkubwa wa marehemu, Ndugu Michael Kwacha Chiume 
(Address : 359 Saunders Drive,Bushkill,
PA,18324) 
ambako ndipo pia alipo Mama Mzazi wa Marehemu hadi hapo taarifa zaidi za lini na wapi taratibu za mwisho zitakapoelekezwa.


Link ya kutoa rambirambi ni : 


Kwa taarifa zaidi wasiliana na:


Michael Chiume:#  646-662-6999
Chris Lutinwa :# 614-592-6231
Nathan Chiume:#  646-552-6347



Dada Jessie atakumbukwa na wengi kwa upole, ukarimu, ucheshi na mapenzi yake kwa Watanzania na wote waliobahatika kumjua. Da Jessie ametuachia pengo kubwa mno. Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema Peponi. AMEEN.

Mungu ametoa, Mungu ametwaa. 


No comments:

Post a Comment