Nani Analipwa mshahara sh. mil 35?

magufuli_aapa

Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’.
Na Mwandishi Wetu, RISASI JUMATANO
DAR ES SALAAM: Baada ya hotuba ya Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ ya Februari 4, mwaka huu, wasomaji wengi wa gazeti hili walipiga simu chumba cha habari na kuuliza kuhusu mtumishi wa umma anayelipwa mshahara wa shilingi milioni 35 kwa mwezi, kama ilivyoelezwa na kiongozi huyo mkuu wa nchi.
RISASI JUMATANO LAINGIA KAZINI
Mara baada ya simu hizo kuzidi kumiminika mfululizo, siku tatu baada ya hotuba hiyo, gazeti hili lilimtafuta Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Utumishi, Anjella Kairuki ili kumtaka atoe ufafanuzi juu ya mtumishi yeyote anayelipwa kiasi hicho kikubwa cha mshahara.
IMG_5400Nehemia Mchechu (NHC)
“Samahani kaka yangu, mimi sihusiki na hilo jambo, siwezi kuongelea kuhusu jambo ambalo tayari rais ameshaliongelea,” alisema waziri huyo.
Risasi Jumatano: Hili jambo halikufafanuliwa na rais, ila alionesha mshangao tu. Sasa kwa vile liko chini ya wizara yako, unaweza kutusaidia.
Kairuki Pichani): Siwezi, kwanza sikuisikiliza hiyo hotuba, lakini pia rais ana wasaidizi wake, mtafute Katibu Mkuu Kiongozi (Ombeni Sefue) atakupa ufafanuzi.
OFISINI KWA KATIBU MKUU KIONGOZI IKULU
Gazeti hili lilifanya mawasiliano na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Ombeni Sefue, lakini lilipoomba kuzungumza naye, mtu wa mapokezi alisema yupo katika ratiba. Hata hivyo, mtu huyo akasema Risasi Jumatano linaweza kuzungumza na mratibu wake aliyemtaja kwa jina la Noel Kaganda.
Kaganda alipoelezwa juu ya nia ya Risasi Jumatano kutaka kujua majina, taasisi au aina ya watu wanaolipwa kiwango cha fedha kilichomshangaza Rais Magufuli, mratibu huyo aliomba mawasiliano ya mwandishi na kuahidi kumtafuta baadaye, lakini hakufanya hivyo hadi alipotafutwa tena siku mbili baadaye.
5 (1)
Felshesmi Mramba wa TANESCO.
“Suala hili ndugu mwandishi nadhani ni vizuri kama ungewasiliana na Msigwa (Grayson, Kaimu Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu) ambaye anashughulika na masuala ya habari. Huyo ndiye hasa mhusika anayeweza kukusaidia katika jambo lako,” alisema mratibu huyo wa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu na kuahidi kumpatia mwandishi wetu namba ya msemaji huyo wa ikulu, jambo alilolitekeleza baada ya sekunde chache.
KUMSIKILIZA MSIGWA, BONYEZA HAPA
“Ndugu mwandishi, alichofanya rais ni kama amekupa tip, ni kazi yako sasa kufuatilia ujue ni mtu gani huyu anayelipwa kiasi hicho cha fedha, kuniuliza mimi ni sawa na wewe kurudi tena kwa rais na kutaka akutajie ni nani huyo anayelipwa kiwango hicho cha fedha.”
Hata baada ya kuelezwa kuhusu juhudi nyingi zilizofanywa ili kupata undani wa suala hilo bila mafanikio, bado Msigwa hakutaka kuzungumza chochote.
“Labda kwa kukusaidia, watafute watu wa Utumishi, wao ndiyo wana orodha ya kila mtumishi wa umma na mishahara yao, wasiliana nao wanaweza kukusaidia.”
UTUMISHI NAKO
Risasi Jumatano halikuchoka, liliwasiliana na Ofisi ya Utumishi wa Umma kwa njia ya simu na kuomba kuzungumza na mtu mwafaka anayeweza kutoa majibu ya kitendawili hicho.
“Hapa hutaweza kumpata mtu wa namna hiyo, nakushauri uwasiliane na watu wa Idara Kuu ya Utumishi huko ndiko unakoweza kupata hicho unachokitafuta,” alisema mwanamke wa mapokezi ambaye alikataa kujitambulisha kwa jina.
d40eDr-Ramadhani-DauRamadhani Dau NSSF.
MSHAHARA NI SIRI
Gazeti hili lilifika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliyopo jijini Dar ambako mtu aliyekuwa mapokezi, baada ya kusikiliza shida ya Risasi Jumatano, alisema:
“Sidhani kama utafanikiwa kaka yangu. Kwa sababu siku zote mshahara wa mtu ni siri yake mwenyewe. Unaweza kuoneshwa au kuambiwa kwa sababu maalum na sidhani kama waandishi ni miongoni mwa watu wanaoweza kuoneshwa mishahara ya watumishi wa umma.”
NI AKINA NANI WANAWEZA KULIPWA HIVYO?
Kwa kawaida, watumishi wengi wa idara za serikali
Baadhi ya wakurugenzi wa mashirika ya umma, idara na taasisi za serikali wanaodhaniwa kuwa miongoni mwa watumishi wa umma wanaolipwa kiwango kikubwa cha fedha ni Nehemia Mchechu (NHC), Ramadhani Dau (NSSF, ambaye sasa ameteuliwa kuwa balozi), Ally Yahya Simba (TCRA), James Mataragio (TPDC), William Urio (PPF), Lutengano Mwakahesya (REA), Philip Saliboko (RITA) na Felshesmi Mramba wa TANESCO.

No comments:

Post a Comment