Marekani, Ulaya zapinga uchaguzi Zanzibar.

Wakati Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, akimtangaza Dk. Ali Mohammed Shein, kushinda uchaguzi wa marudio wa Machi 20, mwaka huu kwa kura 299,982 sawa na asilimia 91.4, Marekani na Umoja wa Ulaya wameeleza kusikitishwa kwao juu ya uchaguzi huo kufanyika bila kuwepo maelewano ya pande zinazokinzana.

Wamesema ili uweze kuaminika na kukubalika ni lazima mchakato wa uchaguzi uwe jumuishi na unaowakilisha kwa dhati matakwa ya watu.

Wakati mabalozi hao wakisema hayo, Rais John Magufuli, amemtumia salamu za pongezi Dk. Shein kufuatia ushindi huo akisema unaonyesha wananchi wanataka awaongoze kwa miaka mingine mitano.

No comments:

Post a Comment