Dar es Salaam. Udhaifu wa sheria zinazosimamia uchimbaji wa Tanzanite umetajwa kuwa chanzo cha madini hayo kuuzwa kwa wingi na nchi za Kenya, India na Afrika Kusini badala ya Tanzania yanakopatikana.
Hayo yalibainika wiki iliyopita katika ziara ya wahariri wa vyombo vya habari kwenye mgodi wa TanzaniteOne Mine Limited (TML), uliopo Mirerani Simanjiro mkoani Manyara.
Mkuu wa Usalama wa TML, George Kisambe alisema ingawa wameimarisha ulinzi kwa asilimia 90 kwa kushirikiana na Stamico chini ya Serikali, udhaifu kwenye sheria unatoa mwanya kwa hujuma dhidi ya Tanzanite na kampuni yao.
No comments:
Post a Comment