Dar es Salaam. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametoa masharti matatu kwa mameneja wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) ili kulinda vibarua vyao.
Akizungumza juzi na mameneja wa wilaya, mikoa na kanda zote nchini, Profesa Muhongo alisema utendaji wao ndiyo utakaowafanya waendelee kuwapo kazini.
Alisema kila baada ya miezi mitatu itakuwa ikifanyika tathmini ya kuangalia utendaji wao.
Miongoni mwa masharti aliyowapa ni kuongeza mapato na idadi ya wateja wanaounganishiwa umeme katika maeneo yao.
No comments:
Post a Comment