Kilango alivuliwa wadhifa huo juzi, akiwa amekalia kiti hicho kwa siku 27 tangu kuapishwa kwake Machi 15, mwaka huu, hivyo kuwa mkuu wa mkoa aliyeweka rekodi ya kukaa muda mfupi katika historia ya Tanzania.
Uamuzi wa Rais Magufuli kumvua Kilango wadhifa huo, ulitokana na kutoa taarifa za uongo juu ya wafanyakazi hewa katika mkoa wake. Kilango katika kikao na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene, alisema katika mkoa wa Shinyanga hakuna hata mtumishi hewa mmoja.
Hata hivyo, Rais Magufuli juzi alisema taarifa hiyo haikuwa ya kweli kwa kuwa imebainika kuwa ndani ya mkoa huo, uchunguzi wa awali unaonyesha kuna watumishi hewa 45 waliosababisha kulipwa Sh. Milioni 339.9.

No comments:
Post a Comment