BALAA USAFIRI WA BURE JIJINI DES SALAAM

Haijapata kutokea kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, kusafirishwa bure, lakini imetokea kwa siku tano mfululizo baada ya kuanza mabasi yaendayo kasi (Udart).
Hata hivyo, bure hiyo ni gharama. Baadhi ya abiria waliotumia usafiri wameshapoteza mali zao kwa vibaka, wameumia kutokana na kubanana huku kukiwa na kundi kubwa la wazururaji ambao husafiri na mabasi hayo bila kushuka popote.
Mbali na bughudha kwa abiria, tayari mabasi hayo mapya yameshaanza kuharibiwa baadhi ya vifaa, kutokana na kukosekana ustaarabu kwa watumiaji. Huo ndiyo usafiri wa mabasi yaendayo haraka.
Awali ilikuwa mabasi hayo yatoe huduma bure kwa siku mbili kabla Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuongeza siku nyingine tatu, ili kuwapa abiria nafasi ya kujifunza zaidi huduma hiyo.
Wakizungumza na mwandishi, baadhi ya abiria walilalamikia kuibuka kwa wimbi la vibaka wa simu na fedha, ambao wamekuwa waking’ang’ania milangoni bila kushuka kwenye vituo.

No comments:

Post a Comment