Machozi! Kwa Nini Mmemchinja Mama Yangu?

DSC_0362Mtoto Allan akiwa amekumbatia picha ya marehemu mama yake, Anethe Msuya.
STORI: MWANDISHI WETU, WIKIENDA
DAR ES SALAAM: ‘Kwa nini mmemchinja mama yangu?’ Ndiyo maneno yaliyokuwa yakimtoka mara kwa mara mtoto, Allan Kimario (4) kila alipokumbuka tukio la mama’ke, Anethe Msuya (30) kuchinjwa shingoni hadi kufa na watu wasiojulikana, nyumbani kwake, Kigamboni, Dar.
KUMBUKUMBU FUPI
Anethe alichinjwa Mei 26, mwaka huu na watu watano waliovamia nyumbani kwake usiku wakiwa wamefunika nyuso kwa soksi nyeusi.
DSC_0388SIKU YA KUAGA MWILI
Mwili wa Anethe ulisafirishwa, Mei 30, mwaka huu kwenda Kijiji cha Kairo, Mererani wilayani Simanjiro, Manyara kwa mazishi baada ya kuagwa kwa machozi yasiyo na mfano huko Salasala jijini Dar. Kwa mujibu wa baadhi ya ndugu wa marehemu, mtoto wake huyo kila alipokuwa akirudiwa na uelewa wa kilichomkuta mzazi wake huyo, alikuwa akiuliza ni kwa nini watu hao walimchinja mama yake?!
“Ni swali gumu kulijibu lakini ukweli ni kuwa, huyu mtoto ameumizwa sana. Mara nyingi amekuwa akilia kwa uchungu na kulala akiwa amekumbatia picha ya mama yake ya enzi ya uhai, jambo lililowatoa watu machozi
msibani.
“Kuna wakati anakuwa kama amesahau na hajui nini kinaendelea, lakini akikumbuka tu, anapoteza amani na uso unakosa furaha. Hasa ndugu anaowafahamu walipokuwa wakilia.”
DSC_0514SWALI LA KILA MARA
“Hata siku ya kuuaga mwili, alikabidhiwa picha moja ya mama yake na akaonekana yupo sawasawa, lakini wakati anapita kuuona mwili huo, alilia na baadaye swali lake lilijirudia tena ni kwa nini walimchinja mama yake?”
kilisema chanzo kimoja juzi baada ya kurejea kutoka mazishini.
MAKUBWA KATIKA MAISHA YAKE
Habari zaidi zinasema kuwa, ukiacha tukio la mama yake kuchinjwa chumbani huku yeye akiwa amelala sebuleni baada ya watu hao kumpulizia dawa inayosadikiwa ni ya usingizi, aliwahi kukumbana na tukio lingine zito. Dada wa Anethe aliyetajwa kwa jina la Antuja inadaiwa kwamba, aliwahi kumwagiwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni sumu wakati akiwa amelala chumbani na mtoto huyo maeneo ya Mbezi-Beach, Dar.
DSC_0501
Mtoto hakuathirika lakini mama mkubwa huyo aliathirika na ikawa ni moja kati ya matukio mengi yaliyoonekana kuiandama familia hiyo.
“Hebu piga picha Allan katika kukua kwake atakuwa na kumbukumbu ya mambo mangapi mazito?” kilihoji chanzo hicho.
KILICHOWAUMIZA WENGI
Wengi wa waombolezaji msibani walikuwa wakimhurumia mtoto huyo kwamba, katika umri mdogo wa miaka 4 amempoteza mama kwa njia ya ukatili huku yeye mwenyewe akili zake zikiwa zinachambua tukio na wakati mwingine kuacha.
DSC_0410“Kama utakumbuka, Allan ndiye aliyekwenda kwa jirani kueleza kwamba, mama yake amelala na kila akimwamsha
haamki wakati yeye anataka kwenda shule.
“Majirani walipokwenda kuchungulia walimkuta amelala chini kwenye dimbwi la damu. Ina maana Allan aliona lakini akili zake zilishindwa kujenga picha kamili kwamba, mama yake amechinjwa na hakuwa hai!
“Na kuna uwezekano mkubwa kwamba, amekuwa akisikia kwa watu wakisemasema kuhusu tukio lile ndiyo maana na yeye linamwingia na kutoka,” kilisema chanzo.
WAFANYAKAZI WENZAKE WAMWAGA MACHOZI
Mamia ya waliofika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Mashariki, Salasala jijini Dar wakiwemo wafanyakazi wenzake wa Wizara ya Fedha alikokuwa akifanya kazi marehemu, walishindwa kujizuia na kuangua vilio walipokuwa wakipita mbele ya jeneza lililokuwa na mwili huo kutoa heshima zao za mwisho.
KIFO CHA KAKA YAKE
Agosti 8, 2013, kaka wa Anethe, ambaye alikuwa mfanyabiashara mkubwa wa madini jijini Arusha, Erasto Msuya ‘Bilionea’, (43) aliuawa kwa kupigwa risasi 22 maeneo ya Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (Kia), Kilimanjaro huku kisasi kikitajwa kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara wenzake. Hivyo, wengi wamekihusisha kifo cha Anethe na kumwagiwa sumu kwa dada yake kama sehemu ya mwendelezo wa kisasi katika familia hiyo.

No comments:

Post a Comment