Prezzo Azidi Kumlipua Jaguar

prezzo (2)BONIPHACE NGUMIJE
MKALI wa Muziki wa Hip Hop Afrika Mashariki, Jackson Makini ‘Prezzo’ hivi karibuni alizidi kulimwagilia maji bifu kati yake na msanii mwenzake kutoka Kenya, Charles Njagua ‘Jaguar’ kwa kudai kuwa hamfahamu na wala hajawahi kumsikia.
jaguarJaguar
Prezzo aliyasema hayo katika Kipindi cha Exclusive kinachorushwa na Global TV Online kuwa jina la Jaguar si geni kwake maana anajua ni aina ya gari au mnyama anayepatikana kwenye misitu mikubwa duniani.
“Huyo Jaguar simfahamu aisee na siku nikija kuambiwa ni msanii nitamshawishi abadilishe jina maana ni ajabu sana binadamu wa kawaida kujiita Jaguar bora hata angejiita Joto!,” alisema Prezzo.

No comments:

Post a Comment