Maganda ya parachichi, ndizi mbivu dawa ya vidonda vya tumbo

avocado-sliced-in-half.jpgLEO kwenye safu hii nitakuletea jinsi unavyoweza kutumia maganda ya ndizi na maganda ya parachichi kujitibu vidonda vya tumbo.
Jinsi ya kuandaa
Chukua parachichi libandue maganda yake, kisha weka kwenye ungo anika ndani kisha chukua maganda ya ndizi pia uanike kwenye ungo ndani, nikisema hivyo namaanisha maganda haya yote hayatakiwi kupata mwanga wa nje, anika ndani mpaka uhakikishe yamekauka. Baada ya kukauka weka kwenye brenda kisha saga maganda yote kwa pamoja upate unga wake.
Matumizi
Ukishapata unga wa maganda hayo tumia kijiko kimoja kikubwa uchanganye na asali kisha urambe. Tumia tiba hii kwa siku mara mbili ni dawa nzuri, wapo waliotumia na kwenda hospitali kupima wakakutwa hawana tatizo la vidonda tena.

No comments:

Post a Comment