Magufuli azima mbwembwe za mastaa kufuturisha


Rais Dk. John Magufuli ‘JPM’

NA HAMIDA HASSAN, Ijumaa
DAR ES SALAAM: Zile mbwembwe ambazo baadhi ya mastaa Bongo walikuwa wakizifanya za kufuturisha kila inapofika kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, safari hii zimezimwa na Serikali ya Rais Dk. John Magufuli ‘JPM’ kufuatia mpango wake wa kubana matumizi.
nishamsaniiNisha
Duru za kihabari zimeeleza kuwa, awali, katika kipindi cha nyuma kulikuwa na mianya ya upatikanaji wa fedha kirahisi kiasi kwamba wakati kama huu ingekuwa ni mwendo wa mastaa kufuturisha huku wengine wakitangaza kwa mbwembwe siku za kufanya hivyo lakini hadi sasa ni kimya.
Wakizungumzia hali ngumu ya maisha, baadhi ya mastaa walisema kuwa, ile jeuri ya kualika watu na kuwafuturisha kwa kutumia gharama kubwa, sasa haipo kutokana na Rais Magufuli kubana upatikanaji fedha kiulaini.
snuramushiSnura.
“Unajua enzi zile unakuta una kigogo wako serikalini, ukimwambia unataka kufuturisha anakuambia andaa bajeti kisha anakupa fedha lakini sasa hivi mambo hayo hakuna, hali ni ngumu na ndiyo maana unaona hadi leo (Jumatano iliyopita) hakuna staa aliyefuturisha kwa mbwembwe,” alisema staa mmoja aliyeomba hifadhi ya jina.
Baadhi ya mastaa waliozungumza na Ijumaa juu ya ishu hiyo walikuwa na haya ya kusema;
Shilole: Pamoja– na huu ugumu wa maisha nikijaliwa nitafuturisha.
Nisha: Natarajia kufuturisha Juni 26, nitafuturu na watoto yatima na watu wasiojiweza pale Mnazi- Mmoja.
Wastara: Maisha ni magumu kweli ila nitafuturisha hata kama siyo kwa mbwembwe.
Snura: Bado sijajua kama nitafuturisha, nikijaliwa inshaallah.
KUMBUKUMBU
Ramadhani iliyopita hadi kumalizika kwa kumi la kwanza baadhi ya mastaa walikuwa wameshafuturisha huku wengine wakitangaza siku za kufanya hivyo lakini safari hii hadi sasa hakuna mbwembwe katika hilo kutokana na upatikani wa ‘fedha za kuchezea’ kuwa mgumu.

No comments:

Post a Comment