Kenya Yaruhusu Uhusiano wa Kimapenzi Baina ya Binamu

kenyaaMahakama Kuu nchini Kenya imehalalisha uhusiano wa kimapenzi baina ya mabinamu kwa kile kilichoelezwa kuwa sababu inakubalika katika baadhi ya jamii nchini humo.
Mahakama hiyo imemuachilia huru mtu mmoja aliyekuwa amefungwa kwa kosa la kushiriki ngono na binamu yake mwaka wa 2014 kwa sababu sio makosa kwa sheria ya nchini humo.
kenyaJaji wa Mahakama Kuu nchini humo, James Makau alisema katika uamuzi kuwa kujamiana kwa maharimu sio haramu nchini Kenya.
”Ibara maalum inachoshughulikia ngono ya maharimu hajata binamu kuwa mmoja wa wale ambao kujamiana nao ni haramu maksudi, kwa sababu baadhi ya jamii nchini Kenya zinaruhusu sio tu ngono bali hata ndoa baina yao”
“Jamii ya Wahindi, Waislamu na baadhi ya makabila nchini Kenya hukubali ndoa baina ya mabinamu” alisema jaji Makau.
Bwana huyo ambaye anatambulika kama Woo alikamatwa mwaka wa 2014 kwa kushiriki ngono na mpenzi wake wa kike ambaye pia ni binamu yake na akahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani.
”Kwa ufupi hakuna ushahidi wowote uliotolewa kuthibitisha kuwa ngono baina ya wawili hao ni kinyume cha sheria na kwa sababu hiyo ninaamuru mtu huyo aachiwe huru mara moja” hukumu ya jaji Makau.

No comments:

Post a Comment