MWANAMKE anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40, amekutwa amekufa katika mazingira yanayoonesha kwamba alibakwa kabla ya kuuawa na kutupwa kichakani. Mwili wake ulionekana Agosti 10, mwaka huu saa 7.30 mchana katika Kijiji cha Iringa Mvumi, Kata ya Mvumi, Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amesema kwamba wanamfanya msako waliotenda unyama...

No comments:
Post a Comment