Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei akimwongoza ukumbini Anna Luambano (33) mkazi wa Kipawa, Dar es Salaam, ambaye anatuhumiwa kuiba mtoto Angle Meck, mwenye umri wa siku kumi. (Picha na John Nditi).
POLISI mkoani Morogoro inamshikilia Anna Luambano (33) ambaye ni mkazi wa Kipawa jijini Dar es Salaam kuwa tuhuma za wizi wa mtoto, Angel Meck mwenye umri wa siku 10 baada ya kumlaghai mama wa mtoto huyo, Maimuna Mahamudu (20) mkazi wa Chamwino katika Manispaa ya Morogoro.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Ulrich Matei amesema wizi huo ulitokea Septemba 13, mwaka huu saa 5 asubuhi katika Mtaa wa Kilimahewa Manispaa ya Morogoro.
No comments:
Post a Comment