Mwanamke mmoja mkazi wa Mikumi wilayani Keya, Mbeya aliyefahamika kwa jina la HILDA SIGARA amefariki dunia akiwa anapelekwa Hospitali kwa matibabu baada ya kupigwa nyundo kichwani na mume wake aitwaye REBSON TWEVE umri kati ya miaka 30 – 35
Kamanda wa polisi mkoani humo DCP Dhahiri Kidavashari amesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 05.01.2017 majira ya saa 12:00 asubuhi ambapo imedaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi kwani inasadikiwa mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.
Amesema katika eneo la tukio kumekutwa nyundo moja, kisu kimoja na fimbo ya muanzi ambavyo vinasadikiwa kutumika katika tukio hilo.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya Kyela ukisubiri kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu na upelelezi unaendelea huku mtuhumiwa akiwa ametoroka mara baada ya tukio na juhudi za kumtafuta zinaendelea.
No comments:
Post a Comment